Share news tips with us here at Hivisasa

Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini watu walihusika katika mauwaji ya Jamaa mwenye akili taahira aliyepigwa risasi Mtongwe wiki  hii.

Naibu kamishana wa Mombasa Akello Odhiambo, alisema siku ya Ijumaa kuwa maafisa wa usalama wanawahoji wakazi wa eneo hilo ili kuwasaidia katika kuwafichua maafisa wanajeshi waliohusika katika mauwaji hayo.

“Maafisa wa polisi wanawahoji na kunakili taarifa kutoka kwa walioshuhudia mauwaji hayoilikusaidia kuwatambua waliohusika,” alisema Odhiambo.

Aidha, ameongeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwanajeshi aliyehusika na mauwaji hayo.

Mwenedazake Ndoro Mwembe mwenye akili tahira anadaiwa kuuwawa kwa akupigwa risasi na wanajeshi kutoka kambi ya Mtongwe alipojaribu kuwashambuliwa kwa mawe.

Mauaji hayo yalizua hisia kali miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu wakiyataja kama mauaji ya kutamausha.