Maafisa was polisi katika kaunti ndogo ya Yatta wameanzisha uchunguzi baada ya mwanamke mmoja was umri wa miaka 47 kupatikana ameuawa nyumbani mwake katika eneo la Matangini katika kaunti ndogo ya Yatta. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akidhibitisha kisa hiki, OCPD wa Yatta Edward Kipsang alielezea kuwa majirani wa mwanamke huyo walimpata akiwa na majeraha ya visu katika uso wake na tumboni. 

Aidha, Kipsang alielezea kuwa wanawe marehemu, anayejulikana kama Philomena Mutinda, ambao ni wa miaka miwili na nne hawakuumizwa. 

"Mshukiwa wa mauaji haya hajapatikana lakini Polisi wamezindua uchunguzi kubaini kiini cha mauaji haya," alisema Kipsang.

Afisa huyo aliwaomba wakazi wa eneo hilo kupiga ripoti iwapo wana habari kuhusu mtu anayeweza kuwa amehusika na mauaji hayo.

"Ningependa wakazi kupiga ripoti iwapo wana habari zinazoweza kusaidia polisi kuzindua mshukiwa was mauaji haya," alisema Kipsang.