Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa polisi katika Kaunti ya Kisii wameombwa kuimarisha usalama katika pande zote za kaunti hiyo haswa sherehe za krismas na mwaka mpya zikikaribia.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa kila wakati sherehe kama hizo zinapowadia, visa vingi hushuhudiwa kufuatia ukosefu wa usalama, na changamoto kutolewa kwa maafisa wa polisi kuhakikisha usalama umeimarishwa ipasavyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii, wakazi wa kaunti hiyo wakiongozwa na Nyanduri Omwenga walisema wanahitaji usalama wa kutosha kutoka kwa maafisa wa polisi haswa katika msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.

“Katika miaka iliyopita tumekuwa tukishuhudia ukosefu wa usalama sherehe zinapowadia kila Desemba kila mwaka huku watu wakichapwa ovyo ovyo. Tunaomba maafisa wa usalama waweze kutuimarishia usalama wetu ili visa hivyo visiwe vinaripotiwa kila mara na kila mwaka,” alisema Omwenga.

Ata hivyo, wakazi hao waliomba maafisa wa polisi kuendelea kufanya msako wa uuzaji wa pombe kwa kile walichokitaja kuwa ni miongoni mwa visa vinavyosababisha ukosefu wa nidhamu na kuleta vurugu miongoni mwa wakazi wa kaunti hiyo.

Ikimbukwe kuwa wiki jana, kamishena wa Kaunti ya Kisii Chege Mwangi alitangaza msako wa pombe unaoendelea katika kaunti hiyo, jambo ambalo limeonekana kuendelea katika baadhi ya sehemu za kaunti hiyo.