Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ili kukabiliana na wahalifu na magaidi katika eneo la Pwani, ni lazima maafisa wa polisi kuihusisha jamii kwa karibu iwapo wana malengo ya kuimarisha usalama eneo hilo.

Afisa mratibu wa mipango katika Shirika la Haki Afrika Francis Auma Gambo amesema kwamba eneo la Pwani inakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa usalama kufuatia kuzembea kwa baadhi ya maafisa wa usalama majukumu yao.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Gamba alisema kwamba maafisa wa polisi wanafaa kubadili mbinu ya kukabiliana na wahalifu kwa kuhusisha jamii karibu ili kupata habari muhimu kuhusu washukiwa wa uhalifu na kuwatia nguvuni.

Gamba alisema kuwa mashirika ya kijamii yatahakikisha kuwa idara ya polisi na jamii zinashirikiana vyema ili eneo hilo la Pwani kuwa na usalama dhabati, huku akisema kwamba hatua hiyo huenda ikasitisha visa vya kihalifu vya mara kwa mara.

"Kuna haja ya maafisa wa polisi kuihusisha jamii katika kupiga vita uhalifu na kuimarisha usalama kwani hiyo ndio njia pekee ya kuuileta jamii pamoja na maafisa wa polisi na kuwasaidia kupata habari muhimu kuhusu washukiwa wa uhalifu na kuwatia nguvuni," alisema Gamba.

Wakati uo huo, imewakosoa maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi na kuhusika katika mauaji ya kiholela dhidi ya watu wasiokuwa na hatia akisema kwamba iwapo hatua hiyo haitasitishwa, basi wakenya wengi watazidi kuangamia.

Kauli ya mwanaharakati huyo imejiri huku wakazi wakilalamikia ukosefu wa usalama katika maeneo yao licha ya idara ya usalama eneo la Pwani kuahidi kuimarisha usalama kwa kiwango kikubwa.