Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baada ya Idara ya Polisi nchini kutoa tahadhari ya kuwepo kwa wafuasi ya ugaidi nchini wanaopanga njama ya kutekeleza mashambulizi, maafisa wa usalama wamezuru mashinani kushika doria kikamilifu.

Afisa mkuu wa Polisi katika eneo la Pwani Francis Wanjohi alisema maafisa wa eneo la Pwani wako macho kuwakabili magaidi wanaolenga kuwahangaisha wakaazi na kuzua hofu ya ukosefu wa usalama miongoni mwao.

Akizungmza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatano, Bw Wanjohi alisema vikosi maalum vya maafisa wa polisi wa kupambana na ugaidi wametumwa kila sehemu katika eneo la Pwani kuimarisha usalama huku akionya atakayepatikana akivuruga usalama wa eneo hilo atakabiliwa kikamilifu.

“Tumetuma kikosi maalum cha kupambana na magaidi mashinani na katika kila sehemu ya eneo hili kuimarisha usalama na maafisa wetu wako macho kupambana na magaidi hao na tunaomba yeyote anayefahamu yule gaidi Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet alisema basi atujulishe mara moja," alisema Wanjohi.