Usalama umeimarishwa kwenye eneo la Maella Naivasha baada ya vurugu kushuhudiwa kwa siku mbili kufuatia mzozo wa kishamba. Mzozo ulikumba shamba hilo baada ya wanachama wa kampuni ya Ng’ati kuvamia wakubwa wao wakidai kuwa wametapeliwa katika ugavi wa ardhi.
Nyumba za mwenyekiti wa Ng’ati ziliteketezwa na vijana waliokuwa na ghadhabu na kusababisha hofu kwenye eneo hilo.
Mkuu wa polisi wa Naivasha Titus Munyoki ameonya wote wanaohusika na uchochezi kuwa watachukuliwa hatua.
Tayari, MCA wa eneo hilo Kariuki Mujina pamoja na washukiwa wengine wametiwa mbaroni.
Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi.