Share news tips with us here at Hivisasa

Raia wa Ujerumani ametozwa faini ya shilingili elfu hamsini ama kifungo cha miezi minne gerezani kwa madai ya kupatikana na tiketi iliyoisha muda wake katika uwanja wa ndege wa Moi jijini Mombasa.

Mahakama imeelezwa kuwa Mark Collins alipatikana katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa Oktoba 29, 2015 akiwa na tiketi hiyo, huku akiwa na nia ya kusafiri hadi Ujerumani.

Mark alikubali makosa hayo siku ya Jumanne na kuiambia mahakama kuwa alikuwa na nia ya kukata tiketi mpya ila maafisa wa polisi wa uwanja huo wakamtia mbaroni.

“Nilikuwa nataka kukata tiketi mpya lakini polisi wakanikamata, sikupanga kutumia tiketi hiyo kusafiri," alisema Collins. 

Mahakama ilimpa raia huyo wa Ujerumani siku 14 kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.