Share news tips with us here at Hivisasa

Huku ziara ya rais Uhuru Kenyatta katika eneo zima la Pwani ikikaribia kukamilika kufika leo, Ijumaa, wakazi wa kaunti hizo watakuwa na kujivunia baada ya rais kuahidi kuanzisha vituo vya urekebishaji tabia katika kila kaunti ili kuwafaidi hasa vijana walioathirika na dawa za kulevya.

Kwenye kongamano aliloandaa siku ya Jumatano na vijana kutoka kaunti mbalimbali kutoka eneo la Pwani katika ikulu ya Rais, Kenyatta aliwahakikishia wakazi kuwa serikali yake itafanya mipango madhubuti ili kujenga vituo hivyo vya kuwasetiri waathiriwa wote husika wa dawa za kulevya katita kaunti hizo za Pwani.

Rais pia alifafanua umuhimu wa jamii kushirikiana na kuwaongoza vijana kutoka Pwani kwa njia ya sawa, na kuwasihi viongozi wote kuanzia wa kidini hadi wale wa siasa kushikana mikono kwa kusudi la kupigana na zongobwingo la matumizi ya mihadarati hali ambayo rais Uhuru alisema sharti ikome ili vijana wajishughulishe kwa masuala ya kuwaendeleza katika maisha.

“Kituo cha urekebishaji kinaanzia kwenye hii na zitajengwa kwa kila kaunti ambayo imeathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya katika mitaa yote na maeneo ya hapam Pwani,” alisema rais.

Ziara ya Rais imekuwa kwa siku tano katika maeneo ya Pwani, na inatajiwa kufika ukingoni siku ya Ijumaa baada ya kukutana na viongozi wa Kaunti ya Lamu.