Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza watalii wakigeni na hata wa humu nchini kuzidi kutalii Kenya bila wasiwasi huku akitaja Kenya kama nchi salama na yenye vivutio vya kupendeza. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Rais alifanya ziara ya ghafla katika bahari ya umma ya Jomo Kenyatta Jumanne usiku na kutangamana na baadhi ya watalii ambapo aliwataka kujihisi nyumbani na kuwa na uhuru wa kuyatembelea maeneo mbali mbali ya vivutio katika mkoa wa Pwani bila kuhofia usalama wao. 

''Karibuni Kenya, nchi yetu ni salama na itasalia kuwa salama kwa hivyo mnaweza zuru sehemu yoyote hapa,ogeleeni baharini na mjihisi nyumbani,'' alisema Rais. 

Akiandamana na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir, mkurugenzi wa kampuni ya kusambaza umeme nchini Ben Chumo na mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mung'aro, Rais, alizuru maeneo ya Mombasa Old Town pamoja na makavazi ya Fort Jesus. 

Kenyatta anatarajiwa kuzindua mradi wa taa mtaani mjini Mombasa kabla kuelekea Nairobi. 

Mradi huo ulifadhiliwa na serikali ya kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na kampuni ya umeme nchini kwa lengo la kuinua uchumi na kuimarisha usalama katika mitaa ya Mombasa.