Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa serikali iko imara kukabiliana na biashara za magendo nchini.

Akizungumza siku ya Alhamisi aliposhudia kuchomwa kwa mali ya thamanai ya mamilioni ya fedha iliyonaswa jijini Mombasa, Kenyatta alisisitiza kuwa wahusika wakuu wa biashara haramu sharti wakabiliwe kisheria kwani inatatiza uchumi wa taifa. 

Siku ya Alhamisi katika eneo la Mwakirunge, serikali iliharibu mali ikiwemo ikiewemo makasha 39 za sukari yenye thamani ya shilling million 56 ya makasha 50 ya mchele.

Siku ya Jumatano, kikosi maalum cha maafisa wa polisi jijini Mombasa walifunga bohari moja katika eneo la Changamwe baada ya kunasa maelfu ya magunia ya mchele na nafaka nyengine zenye thamani ya mamilioni ya fedha zinazoaminika kupitwa na wakati wake wa matumizi.

Mratibu mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa alisema magunia hayo yaliingizwa humu nchini kutoka milki ya Kiarabu, na mchele huo ulikuwa ukipakiwa upya katika mifuko mingine kuuzwa.