Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya Kisii Jimmy Angwenyi amemwomba Rais Uhuru Kenyatta kutomsimamisha kazi waziri wa serikali za ugatuzi Ann Waiguru jinsi ameombwa na idadi kubwa ya viongozi nchini.

Mwanasheria huyo alisema Waiguru hajapatikana na makosa ya kuhusishwa na ufisadi, ila ni madai na sharti uchunguzwe kabla ya kumfuta kazi.

Akizungumza katika eneo bunge lake siku ya Jumanne, Angwenyi aliomwomba Kenyatta kutofuata na yale anaagizwa kufanya kwani Waiguru ndiye alikuwa wa kwanza kupiga kamsa ya pesa kuipiwa kutoka wizara yake .

“Naomba Rais Kenyatta kutomfuta kazi Waiguru maana hajapatikana na makosa, na sharti achunguzwe kikamilifu, na ninatumai hawezi kuwa na makosa,” alisema Angwenyi

Aidha, mbunge huyo alisema kuwa Waiguru anafuatwa na kutafutwa kisiasa, jambo ambalo halina msingi wowote, na kuomba viongozi kuenda pole pole ili kubaini ukweli halisi wa mambo.

Hapo awali, viongozi wa muungano wa Cord walimtaka Waiguru kuondoka afisini ili kuchunguzwa na tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC, lakini kufikia sasa baadhi ya viongozi wa muungano wa Jubelee nao wamemtaka Waiguru kujiondoa afisini ili kuchunguzwa.

Ikumbukwe kuwa juma lililopita, mbunge wa Nandi Hills Alfred Ketter alipeleka mswada wa kumtimua mamlakani waziri Waiguru,  lakini spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi akaufutilia mbali mswada huo kutojadiliwa kwa kile kilichosemekana kutokuwa na ushahidi wa kutosha.