Hatua ya mrengo wa Jubilee kuvileta pamoja vyama vyake kwa ajili ya umoja wa taifa kamwe haiwezi kuzuiliwa, hii ni kwa mjibu wa naibu wa rais William Ruto.
Ruto amesema kuwa serikali inasikitika sana kuhusiana na suala la baadhi ya viongozi kuwagawanya wananchi kwa misingi ya kisiasa.
Ruto ameonya kuwa serikali ya Jubilee haitokubali migawanyo ya kisiasa na kikabila na vile vile kuenezwa kwa chuki miongoni mwa makabila mbalimbali.
"Sisi kama Jubilee tumeamua na hatutarudi nyuma kwa siasa ya karne ya zamani, siasa duni ya mugawanyiko kikabila, hiyo siasa haitawezekana tena," Ruto alisisitiza
Ruto alikuwa akizungumza siku ya Jumapili katika hafla ya kutoa shukrani kwa waziri wa kilimo William Bett katika shule ya upili ya Kapsabet, kaunti ya Nandi.
Baadhi ya waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago, mwezake Cleophas Lagat wa Nandi miongoni mwa viongozi wengine.