Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Naibu wa Rais William Ruto anatarajiwa kujua hatima yake siku ya Ijumaa 12, 2016 katika kesi ya jinai dhidi yake ambayo inamkumba katika mahakama ya ICC. 

Hili lilithibitishwa siku ya Jumatatu jioni na mahakama ya kukata rufaa.

Siku hiyo, mahakama itatoa uamuzi wa iwapo ilikuwa sawa majaji kutumia ushahidi wa mashahidi ambao tayari walijiondoa katika kesi hiyo.

Hili linajiri baada ya uamuzi wa hapo awali wa kiongozi wa mahakama hiyo Fatou Bensouda kusema kuwa ilikuwa sawa kwa mahakama kutumia ushahidi huo.

Hata hivyo uamuzi huo ulikumbwa na changamoto pale baadhi ya mashahidi walijitokeza na kusema kuwa ushahidi wao ulikuwa wa uongo.

Kwenye taarifa ya mwisho ya mashahidi, Bensouda alitetea kuwa mashahidi walisema kuwa ushahidi wao ulikuwa wa uongo kutokana na vitisho walivyokuwa wakipokea kutoka kwa wahusika na hivyo kusisitiza kuwa ushahidi huo ni wa muhimu na ni sharti utumike.