Huenda sekta ya utalii nchini ikaimarika hata zaidi baada ya Kenya kupata ithibati ya kuanzisha safari za ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Marekani kuanzia mwezi Mei mwaka huu. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni kufuatia ripoti ya ukaguzi uliofanywa na shirikia la kimataifa linalohusika na utafiti wa viwanja vya ndege duniani maarufu kama 'International Aviation Organisation' ikishirikiana na shirika la ndege nchini, kubaini kuwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta upo katika ubora wa kimataifa. 

Kulingana na ripoti hiyo iliyofanywa kati ya Septemba 17 na 24, 2014, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta umehitimu kwa asilimia 88, hii ikiwa ni asilimia 8 zaidi ya kiwango kilichowekwa. 

Akithibitisha haya, waziri wa uchukuzi James Macharia alisema hii ni hafueni kwa Kenya kwani imekuwa ikijaribu kufikia kiwangu hicho tangu 2013 bila mafanikio. 

''2013 tulikuwa na asilimia 66, 2014 tukawa na asilimia 78.42 lakini mwaka huu tumehitimu,'' akasema waziri. 

Hii ni baada ya uwanja huo kufanyiwa ukarabati ambapo shiriki la ndge nchini lilitumia Shilingi bilioni 9 huku serikali ikitoa shilingi bilioni 1.3. 

Safari hizo zinatarajiwa kuanza mwezi Mei, 2016, huku wadau wa sekta ya utalii nchini hususan kutoka mkoa wa Pwani, wakiwa mwingi wa matumaini kuwa sekta hiyo itaimarika kwani watalii wataweza kusafiri moja kwa moja kutoka Marekani hadi nchini. 

Mwaka wa 2015 watalii wengi walizuru nchini ikilinganishwa na 2014 kufuatia hatua ya mataifa ya Uingereza, Marekani na Ufaransa kuondoa vikwazo vya usafiri iliyowawekea wananchi wake baada ya kuimarika kwa usalama nchini.