Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwekahazina wa chama cha maendeleo ya wanawake kaunti ya Nakuru Florence Chepkorir amewataka wakaazi wa kaunti ya Nakuru kuzingatia amani na umoja kila wakati kama walivyodumisha amani wakaazi wa kaunti ya Kericho wakati wa uchaguzi mdogo wa kumchagua seneta wa kaunti hiyo.

Akizungumza huko Kaptembwa eneo bunge la Nakuru Magaribi Chepkorir alisema kuwa wakenya hawako tayari kugawanywa na badala yake wanataka maendeleo.

Vilevile alitoa wito kwa seneta huyo ambaye alichaguliwa kwa tiketi ya chama cha JAP kuhakikisha anawafanyia wakaazi wa kaunti ya Kericho kazi kwa usawa pasi na kuweka mipaka.

Kadhalika mweka hazina huyo alisisitiza kwamba jamii ya Kelnjin ni kitu kimoja huku akikanusha madai ya baadhi ya watu kuwa jamii hiyo imegawanyika kisiasa.