Seneta wa kaunti ya Nyamira Mong’are Okong'o amejitokeza kushtumu vikali ripoti kuwa amekuwa akisambaza kalamu zisizo na wino katika shule mbalimbali kaunti ya Nyamira. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na Mongare, ripoti hizo ni za baadhi ya mahasimu wake wa kisiasa walio na nia ya kumharibia jina, huku akiwahimiza wakazi wa kaunti hiyo kupuuza madai hayo. 

"Kwa kweli nimekuwa nikipokea simu za madai ya kusambaza kalamu zisizo na wino, ila ni ombi langu kwa wakazi wa kaunti ya Nyamira kupuuza madai hayo kwa kuwa hizo ni propaganda za wanasiasa wapinzani wa uongozi wangu walio na nia ya kuniharibia jina," alisema Mongare. 

Mongare aidha aliwapa changamoto wanasiasa wanaoibua madai hayo huku akiongezea kuwa hamna shule hata moja alizo zipokeza kalamu iliyo jitokeza kulalamikia hali hiyo. 

"Wale watu wanaosambaza madai hayo kuwa nimekuwa nikipokeza shule mbalimbali kalamu bila wino wacha wajue kwamba hawana nafasi ya kuniharibia jina hata kidogo kwa kuwa hamna shule hata moja ambayo imewasilisha madai hayo kwangu," aliongezea Mongare.