Vijana ambao hawakuafikia alama zakuwawezesha kujiunga na vyuo vikuu nchini kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne wameombwa kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kujistawisha. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya ni kulingana na seneta wa kaunti ya Nyamira Mong’are Okong'o aliyekuwa akihutubu kwenye hafla ya kuchangisha pesa za kuwasaidia wahudumu wa bodaboda kule Nyamusi siku ya Jumamosi, aliposema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu ni chache sana. 

"Serikali ya kaunti ya Nyamira imewekeza pakubwa katika vyuo vya kiufundi, na nihimizo langu kwa vijana ambao hawakuweza kupata alama za kuwawezesha kujiunga na vyuo anuwai na vile vikuu kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kupata maarifa yatakayo wasaidia maishani," alisema Okong'o. 

Seneta Okong'o aidha aliwaonya vijana dhidi ya kujiuhusisha na uhalifu huku akiwatakaa machifu na manaibu wao kushirikiana na maafisa wa polisi ili kuwatia mbaroni wahusika. 

"Ningependa kuwahimiza vijana kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kupata maarifa ya taaluma mbalimbali ambayo yanaweza wafaa maishani badala ya kuwapora wananchi mali yao na ndio maana nawataka maafisa wa utawala kushirikiana na maafisa wa polisi ili kuwanasa wahalifu," aliongezea Okong'o.

Picha: Seneta wa kaunti ya Nyamira Okong'o Mogeni. Amewahimiza vijana wengi wa kaunti yake ambao hawakufanya vyema katika mtihani wa KCSE kujiunga na vyuo vya kiufundi. Maktaba