Serikali inapania kutumia kima cha shilingi bilioni 1.2 kufufua sekta ya utalii katika upande wa fuo za bahari, kwa mujibu wa waziri wa utalii Najibu Balala.
Akizungumza siku ya Jumanne wakati wa ufunguzi wa hoteli ya kimataifa ya English Point Marina katika eneo bunge la Nyali, Balala alisema kuwa hatua hiyo itaimarisha pakubwa biashara ya utalii ambayo aimeitaja kuimarika kwa sasa.
Aidha, Balala amesema kuwa katika hatua hiyo ya kuimarisha utali wameondoa ada ya maegesho ya ndege katika viwanja vya Mombasa na Malindi.
Wakati huo huo waziri huyo wa utalii amesema kuwa ili kuvutia wawekezaji zaidi humu nchini sambamba na kuimarisha sekta ya utalii lazima wananchi na viongozi kuachana na swala la kutoa changamoto za ukosefu wa usalama nchini.
Balala amesema kuwa hatua hiyo inarudisha nyuma taifa kwani wawekezaji wengi hurudi nyuma wakati wanaposikia changamoto zinazokumba maeneo ya uwekezaji.