Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kujenga ua katika soko la Market lililoko katikati mwa mji wa Kisii ili kuimarisha usalama wa bidhaa za wafanyibiashara hasua nyakati za usiku.
Kulingana na wafanyibiashara hao, wengi wao huacha mizigo yao hapo ili kuamkia siku ifuatayo na kuendeleza biashara zao, jambo ambalo wameanza kulihofia kwani huenda wakapoteza bidhaa zao kwa kuwa soko hilo halina ua la kudumu.
Wakiongea na waandishi wa habari siku ya ijumaa, wafanyibiashara hao wakiongozwa na Jurius Kombo, wameiomba serikali ya kaunti kupitia idara ya biashara, ardhi na ya mpangilio wa mji kujenga ua ili kuimarisha usalama.
Pia, wanataka ujenzi huo kuharakishwa kwani si mara ya kwanza wameiomba serikali hiyo kujenga ua hilo.
Waliongezea kuwa ua utasaidia kuepusha baadhi ya wamiliki wa magari ambao wamekuwa wakiyaegesha magari yao kiholelaholela na kuharibu bidhaa zao.
“Tunaomba serikali ya kaunti iitikie ombi letu maana tunatozwa ushuru kila siku na tunaomba tujengewe ua ilituhakikishiwe usalama wa bidhaa zetu,” aliongezea Julius Nyakundi.
“Soko hili limekuwa likiachwa nyuma kwa muda mrefu kwa maendeleo tunaomba serikali ya kaunti iwze kutukumbuka,” aliongeza Nyakundi