Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kitaifa imelahumiwa vikali kwa kudaiwa kutumia mamlaka kufanya ufisadi kujitafutia pesa ambazo itatumia kufanya kampeni katika uchaguzi mkuu mwaka ujao 2017.

Kulingana na kiongozi wa muungano wa upinzani CORD Raila Odinga, serikali ya kitaifa inafanya ufisadi kupata na kujitayarisha kufanya kampeini mwaka ujao kwa kutumia pesa za ufisadi.

Aidha, Odinga alisema si vizuri kwa serikali kutumia raslimali za wakenya kujinufaisha wenyewe, huku akiongeza kuwa hilo ni kukiuka sheria.

Akiongea siku ya Alhamisi mjini Kisii wakati alihudhuria kongamano la wafanyibiashara, Odinga alilaumu serikali kwa kuendelea kuhusika na ufisadi na kutumia mamlaka yao vibaya.

“Serikali ya kitaifa imejulikana yale inaendela kuyatenda maana inafanya ufisadi kutafuta pesa na kuweka mahali ili kutumia mwaka ujao kufanya kampeini na hilo ni kinyume na sheria,” alisema Odinga.

Wakati huo huo, Odinga aliomba magavana wote nchini kujaribu kila wawezalo kuhakikisha maendeleo yamefanywa kikamilifu katika kaunti zao ili kunufaisha wakazi

“Naomba magavana kufanya maendeleo kwa wakazi maana mlichaguliwa kufanya maendeleo, kile ninaomba msihusike kwa ufisadi kama serikali ya kitaifa inaendelea kuhusika kila siku kila wakati,” aliongeza Odinga.