Serikali ya kaunti ya Nyamira imekosolewa vikali kwa utumizi mbaya wa fedha za umma, badala ya kutumia pesa hizo kufanya maendelo.
Hii ni baada ya kubainika kuwa serikali ya kaunti hiyo ilitumia millioni 2.8 kununua maziwa, maji na soda ambazo wafanyikazi wa serikali hiyo wanakunywa wakiwa afisini.
Haya yalifichuka baada ya gavana wa kaunti ya hiyo John Nyagarama kufika mbele ya kamati ya seneti kuhusu utumizi wa pesa za umma siku ya Alhamisi na kutakiwa kutumia pesa vizuri kufanya maendeleo badala ya kujistarehesha.
Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Alhamisi mjini Nyamira, wakazi wa kaunti hiyo wakiongozwa na George Morara baada ya kupokea yaliyojiri kati ya gavana na kamati ya seneti waliomba gavana kutumia pesa kukarabati barabara badala ya kujistarehesha na wafanyikazi wake.
“Millini 2.8 ni pesa nyingi ambazo gavana wetu angetumia kufanya maendeleo badala ya kununua vinywaji kwa wafanyikazi wake,” alisema Morara.
“Sisi tulimchagua atufanyie maendeleo na sio kujistarehesha jinsi anafanya na wafanyikazi wake,” aliongeza Martha Moreka, mkazi mwingine.
Aidha, kamati hiyo ya seneti iliwakosoa wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Nyamira kwa kukabidhiwa millioni moja kila mmoja ili kupangisha nyumba za kifahali pa kulala na kutakiwa kuzirudisha pesa hizo kufanya maendeleo kwani wengi hutoka makwao
“Tunahitaji pesa hizo zirudishwe kutengeneza hospitali zetu na kunua dawa pamoja na kukarabati barabara.