Mwenyekiti wa Shirika la kijamii la National Citizen Engagement Forum (NACEF) Moses Gitonga, ametoa wito kwa serikali kutatua kwa haraka migogoro katika sekta ya elimu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katika mahojiano na mwandishi huyu siku ya Alhamisi, Gitonga aliema ni jambo la kusikitisha kwamba sekta ya elimu inaendelea kukumbwa na changamoto kama vile migomo, kupandishwa karo na pia wizi wa mitihani ya kitaifa.

"Serikali inafaa kuwajibika na kutatua migogoro hii ambayo inayumbisha sekta ya elimu,” alisema Gitonga.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa taifa hili limepiga hatua kadhaa kwa kupitisha katiba ambayo inatoa fursa kwa kila mtoto kupata elimu bora.

Kwa mujibu wake, iwapo gharama ya masomo itakuwa juu kuliko kipato cha wazazi, basi hiyo itakua ni ukiukwaji wa sheria na haki za watoto.

Gitonga ametoa wito kwa Waziri wa Elimu Dr Fred Matiangi kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inazidi kuimarishwa.