Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wananchi waliokusanyika nje ya chumba kimoja cha kuhifadhi maiti jijini Nakuru walikumbwa na mshtuko siku ya Jumamosi baada ya amri kutolewa ya kusitisha mazishi ya marehemu Alfred Leshau.

Watu hao kutoka jamii ya Maasai walishangazwa kupata amri kutoka kwa Kamanda wa kaunti ya Nakuru Hassan Barua, mzozo ukiwa ni wa ardhi. 

Kampuni ya ADC Farm awali iliwasilisha kesi kortini kusitisha shughuli hiyo ikidai kuwa wamiliki wa shamba tata ambayo marehamu alikuwa azikwe.

Hata hivyo, wakili wa familia hiyo Martin Ole Kamwaro akiwahutubia wananchi wa jamii hiyo Naivasha ameahidi kufuatilia kesi hiyo hadi pale hali itakapotendeka kwa familia hiyo ya marehemu.

"Tulipata taarifa hii pindi tulipowasili kuchukua maiti huyu kuwa haturuhusiwi kumzika mwenzetu kwa sababu shamba tulilopanga kumzika ina mzozo wa umiliki. Wiki ijayo tutaenda kortini kupinga amri hii ambayo inanuia kunyang’anya familia ya marehemu shamba yao," Kamwaro alielezea.

Viongozi mbalimbali waliokuwemo hapo wakiongozwa na mwanyekiti wa chama cha ODM tawi la Nakuru Peter Ole Osono pia walikashifu amri hiyo wakiitaja kama njia mojawapo ya kunyanyasa watu wa jamii hiyo.

"Serikali inahitaji kuwajibika na kulinda wananchi dhidi ya wanyakuzi wa shamba za watu haswa jamii ya Maasai ambayo inaendelea kudhukumiwa," Ole Osono alielezea.