Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema serikali yake imeupa mradi wa kukarabati barabara kipau mbele ili kurahisisha sekta ya uchukuzi kwa wakulima na wafanyibiashara.

Kulingana na gavana Ongwae, wafanyibiashara ndio na wakulima huchangia zaidi kuinuka kwa uchumi katika kaunti hiyo na kuleta maendeleo, na kusema sharti wakarabatiwe barabara ili wapate mahala pa kupita na kuendeleza shughuli zao za biashara.

Akizungumza mjini Kisii siku ya Jumatano, gavana Ongwae alisema barabara zote zile ziko nchini ya uongozi wa kaunti hiyo zitakarabatiwa hivi karibuni ili wafanyibiashara kupata mahala pa kupita.

Ongwae aliongeza kuwa serikali yake imeupa mradi wa ukarabati wa barabara kipau mbele, huku miradi mingine ikifuata.

“Serikali yangu kila mwaka inatenga pesa kwa ukarabati wa barabara kwa kilomita 45, na tangu niingie afisini kama gavana, nimekuwa nikikarabati barabara na ninaenda kukarabati zingine mwaka huu ili sekta ya uchukuzi iwe shwali,” alisema gavana Ongwae.

Pia gavana huyo aliwaomba wabunge wote tisa wa kaunti hiyo pamoja na wawakilishi wa kaunti kushirikiana kuhakikisha sekta ya uchukuzi imeinuka kwa kukarabati barabara ili wanabiashara kupata mahala pa kupitisha mizigo yao.

“Kuna baadhi ya wabunge ambao bado hawajaweka kando maswala ya uchaguzi uliopita wa mwaka wa 2013 kwa kufuata vyama vya kisiasa, hilo halitajenga nchi kamwe, na ninawaomba tufanye kazi pamoja,” aliongeza Ongwae.