Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa eneo bunge la Kitutu Chache kusini Kaunti ya Kisii Richard Onyonka ameomba serikali ya kitaifa kuanzisha mradi wa huduma kwa vijana katika kila eneo bunge humu nchini ili kusaidia idadi kubwa ya vijana kujiendeleza kimaisha.

Onyonka alitoa ombi hilo baada ya kubainika kuwa mradi huo wa NYS unatoa usaidizi mkubwa kwa vijana haswa wale hawana kazi za ajira na kupata riziki ya kila siku.

Akizungumza mnamo siku ya Jumapili mjini Kisii, Onyonka alisema mradi wa NYS una ufanisi mkubwa kwa vijana, huku akisema kuna haja ya serikali kuanzisha mradi huo kila eneo bunge nchini na kusaidia vijana wengi.

Napongeza serikali ya kitaifa kwa kuleta mradi wa NYS maana umetoa usaidizi kwa vijana wetu ambao hawakuwa na ajira na wameoneka kujiendeleza kimaisha,” alisema Onyonka.

“Naomba serikali jinsi ilianzisha mradi huo katika baadhi ya maeneo bunge, naomba ianzishe kwa maeneo bunge yote ili kusaidia idadi kubwa ya vijana ili kujiendeleza na kujiimarisha kimaisha,” aliongeza Onyonka.

Wakati huo huo, Onyoga alipongeza serikali kwa kurudisha mradi huo baada ya kusimimishwa kwa muda kufuatia sakata iliyokumba mradi huo iliyodaiwa kuwa ya ufisadi .

“Naomba serikali iwape pesa ambazo ilikuwa inawakata vijana wa NYS hapo awali ambazo zilisemekana kuwekwa kwa Sacco yao ili nao wapata pesa zao na wafanyie kile wanahitaji,” alihoji Onyonka.