Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini kaunti ya Kisii wameomba serikali ya kaunti hiyo kupandisha hospitali ya Marani iliyoko mjini humo hadi level Five ili kutoa huduma bora za matibabu ikilinganishwa na huduma zinazotolewa kwa sasa.

Kulingana na wakaazi hao huduma za matibabu zinazotolewa katika hospitali hiyo ya Marani hazipendezi na kuomba msaada kutoka kwa serikali ya kaunti ili kuipandisha hospitali hiyo na kuongeza wahudumu wa kutoa matibabu kama njia mojawapo ya kuimarisha sekta ya afya na huduma bora.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Marani, wakaazi hao wakiongozwa na Jonathan Nyasikera walisema huduma za matibabu zinazotolewa katika hospitali ya Marani hazipendezi kutokana na ukosefu wa madaktari wa kutosha na kuomba ipandishwe hadi level 5.

“Huduma ya matibabu ambayo tunapokea hapa Marani haipendezi na tunaomba serikali ya kaunti ipandishe hospitali hadi level five ili huduma iweze kubadilika wakati mwingine tunapoenda level 6 mjini Kisii kuna msongamano mkubwa,” alisema Jonathan Nyasikera.

Aidha, wakaazi hao walisema hospitali hiyo iko level 4 lakini mara nyingi hukosa dawa na kulazimika kununua dawa kutoka zahanati ili kutumika kutoa matibabu.

“Huduma ya matibabu inayotolewa hapa Marani haipendezi tunaomba serikali iwe inaongeza dawa kila wakati na iongeze madktari ili huduma hiyo iimarike,” alisema Gladys Ochoi mkaazi.