Askofu wa kanisa la Word of Faith Church International iliyoko eneo la Daraja Mbili mjini Kisii Isaac ameiomba serikali ya kitaifa kujitokeza na kueleza wakenya ruwaza ya mwaka wa 2030 imefikia wapi ili wakenya kujua penye nchi inakotoka na inakoelekea.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano mjini Kisii, Waire aliiomba serikali kuwaeleza wakenya penye ruwaza ya 2030 imefikia, na ni kipi kinastahili kutarajiwa kabla ya mwaka huo kufika.
Kulingana naye, idadi kubwa ya wakenya hawajui penye nchi inakoelekea kufuatia visa vya ufisadi ambavyo vimeonekana kuongezeka kila kuchao, huku akihofia kuwa huenda yale yalitarajiwa kuafikiwa yagonge mwamba.
“Tuliambiwa na serikali hapo mbeleni kuwa kufikia mwaka wa 2030 tutakuwa na matarajio mengi ya maendeleo ambayo yatakuwa tayari yamefanywa humu nchini, lakini kufuatia ongezeko la visa vya ufisadi, hatujui penye nchi inaenda,” alisema Waire
“Naomba serikali kuu kutueleza bayana tuko wapi na tunakoelekea ni wapi, kila mradi ambao unaanzishwa humu nchini unastahili kuwa na mikakati kabambe ili kutoteleza na kuangamiza wahusika,” aliongezea.
Hata hivyo, aliomba wakenya kuishi kwa amani na kuweka kando masuala ya ukabila na kuendelea kuombena ili kusukuma gurudumu la maisha mbele wakiwa pamoja.
Askofu huyo aliomba viongozi walio mamlakanmi kufanya kazi na umoja ili kuwatumikia wakenya kulingana na yale waliyowahidi.