Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti katika kiwanda cha majani chai cha Kebirigo David Kireri ameiomba serikali kupunguza ushuru zinazotozwa wakulima wa majani chai ili mkulima wa mumea huo kuendelea kufaidika.

Kulingana na mwenyekiti huyo, wakulima hupata hasara kwani wanatozwa zaidi ya ushuru wa shilingi ishirini kabla ya pesa zao kuwafikia, jambo ambalo amesema halifurahishi kamwe, na kuomba ushuru kupunguzwa ili kufaidi mkulima wa mumea huo.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii, Kireri alisema wakulima wamesumbuka sana kwa kukatwa pesa nyingi kama ushuru, jambo ambalo haliwafaidi wakulima hao vyovyote.

Aidha, alisema wakulima hupata hasara kwa majani chai yao kwani hukaa kwa vituo vya ununuzi kwa muda mrefu bila kuchukuliwa kufuatia barabara mbovu ambazo hazipitiki.

Kireri alisema yanayosababisha kutochukuliwa kwa majani chai hayo ni vile serikali ya kitaifa iliondoa pesa zile zilikuwa zinagharamia ukarabati wa barabara kutoka viwanda mbalimbali, huku akiomba pesa zile zilikuwa nchini ya halmashauri ya KTDA zirudishwe ili zitumiuke kukarabati barabara jinsi ilivyokuwa hapo awali.

“Hapo awali halmashauri ya KTDA ilikuwa na pesa fulani ambazo zilikuwa zinakarabati barabara za kuelekea vituo vya ununuzi pamoja na viwanda, lakini serikali iliondoa pesa hizo,” alisema Kireri.

“Tunaomba seriakali irudishe pesa hizo kwani barabara hizo zimeharibika pakubwa, jambo ambalo hupelekea majani chai hayo kutofika kwa viwanda mapema kufuatia barabara mbovu ambazo hazipitiki,” aliongezea.