Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa chama cha Kenya National Congress (KNC) Atati Kengere ameiomba serikali kuwalipa wakimbizi wa ndani katika kaunti za Kisii na Nyamira kama sehemu zingine za nchi ili kuonyesha uwazi kwa wananchi wote kwa ujumla.

Kulingana na Kengere, ni haki ya wakimbizi kulipwa pesa zao kwani ghasia zilizozuka mwaka wa 2007 na 2008 ziliwasababishia hasara kubwa na kuwaacha wengi wa jamii ya mkisii kufurushwa kutoka walikokua.

Akizungumza siku ya Jumanne katika mkahawa mmoja mjini Kisii, Kengere alisema kabila zingine humu nchini tayari zimelipwa, huku kabila ya mkisii ikisalia kutolipwa hadi sasa.

“Naomba serikali iwalipe wakimbizi wa ndani wa jamii ya mkisii jinsi ilivyowalipa kabila zingine za nchi. Ikiwa serikali inajali maslahi ya wakenya wote sharti iwahudumie wote kwa njia uwazi,” alisema Kengere.

Wakati huo huo, Kengere alisema wakati umefika kila mwananchi anastahili kupata haki yake ili kufaidika kutoka kwa serikali ya Kenya

Pia Kengere aliomba serikali kufanya maendeleo mengi katika Kaunti za Kisii na Nyamira ili kufadi wakisii.

“Naomba serikali kutimiza ahadi ilizotoa za maendeleo ili kufahidi jamii ya mkisii na kufurahia matunda ya serikali,” aliongeza Kengere.