Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kitaifa imeombwa kuanza kuwalipa wasimamizi wa mradi wa Nyumba kumi kama njia moja ya kuimarisha usalama katika vijiji mbalimbali nchini.

Ombi hilo lilitolewa baada ya kubainika kuwa kwa muda mrefu wasimamizi wa mradi huo wa Nyumba Kumi wamekuwa wakitoa usalama katika vijiji mbalimbali bila kupewa chochote cha kujikimu kimaisha jambo ambalo sasa limepingwa.

Akizungumza na mwandishi huyu mnamo siku ya Jumatatu mjini Kisii mwenyekiti wa chama cha Kenya National congress [KNC]Atati Kengere alisema kuna haja kwa serikali ya kitaifa kuanza kuwalipa wasimamizi wa mradi wa Nyumba kumi ili kuwapa motisha ya kuendelea kuimarisha usalama katika vijiji mbalimbali nchini.

“Mradi wa Nyumba kumi ulianzishwa ili kuleta usalama katika vijiji mbalimbali kama njia moja ya kupunguza visa vya uhalifu katikia vijiji na mradi huo ulipokelewa kwa moyo mmoja,” alisema atati Kengere

“mtu anapotoa usaidizi naye anastahili kusaidiwa . Naomba serikali kuanza kuwalipa wale wasimamizi wa mradi huo wa Nyumba kumi ili nao waweze kujikimu kimaisha

Pia kengere alisema mtu awezi kuweka usalama katika mahali fulani bila kulipwa chochote na kusema ni haki kwa wasimamizi wa mradi huo kupata mshahara kama wasimamizi wengine katika vitengo vya usalama hulipwa nchini ili kuonyesha uwazi.