Share news tips with us here at Hivisasa

Kutokana na ongezeko la vijana kujihusisha na itikadi kali, serikali imetakiwa kuja na mbinu tofauti katika kukabiliana na vita dhidi ya misimamo mikali miongoni mwa vijana kwani njia inayotumika kwa sasa haijafikia kiwango kinachostahili.

Haya ni kulingana na mhadhiri katika chuo kikuu cha pwani daktari Athman Mujjahid.

Mujjahid alisema siku ya Jumanne kuwa njia inayotumika inazidi kuwapa motisha wale walioathirika na misimamo mikali.

Aliongeza kuwa familia nyingi zimeshindwa kuwapa mafunzo mema watoto wao kwa sababu ya utandawazi pamoja na wazazi kutotenga muda na watoto, akitaja kuwa wengi wao hutumia muda mwingi kazini na hata wengine kuwa kikazi ughaibuni.

Mujahid aliyasema haya katika kongamano la kuhamasisha vijana dhidi ya misimamo mikali ya kigaidi lilioandaliwa na shirika la kijamii la KECOSCE.

Takriban vijana mia tatu kutoka eneo bunge la Nyali walihudhuria kongamano hilo.