Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku msimu wa upanzi uking’oa nanga katika sehemu mbalimbali nchini serikali imeombwa kupunguza bei ya mbegu za mahindi.

Hii ni baada ya bei ya mbegu hiyo kupandishwa kupita kiasi katika maduka mengi katika kaunti ya Kisii na kuwa vigumu kwa wakulima hao kununua mbegu hiyo kwa wingi.

Wakizungumza leo mjini Kisii, wakulima wa mahindi katika kaunti hiyo walisema gharama ya mbegu hiyo imepandishwa zaidi kutoka Sh240 bei ya awali hadi Sh350 kwa kilo mbili na kutatiza shughuli zao za upanzi.

 Wameomba serikali kujaribu kila iwezalo kuhakikisha bei hiyo imepunguzwa.

"Kama serikali inahitaji kutusaidia sisi wakulima tunaomba itupunguzie bei ya mbegu ya mahindi ili tuweze kufanya kilimo chetu kwa wingi maana tusipopanda mbegu kwa wingi huenda janga la njaa likaibuka hapa Kisii," alisema Mokami.

Pia wakulima hao waliomba serikali kupunguza zaidi bei ya mbolea na kuisambaza katika sehemu zote za kaunti za kisii na Nyamira ambapo kilimo cha mahindi hufanyika kwa wingi .