Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali imetakiwa kuwajibika ili kutatua msongamano unaoshuhudiwa mara kwa mara katika Kivuko cha Likoni.

Hii ni baada ya wadau katika sekta ya utalii waliofanya kikao na wakuu wa bodi ya kivuko cha feri na kuitaka serikali kuwajibika ili kutatua tatizo la msongamano wa magari na abiria unaokumba kivuko hicho mara kwa mara.

Akihutubia waandishi wa habari Jumatau, baada ya kikao hicho, naibu mwenyekiti wa muungano wa watalii eneo la Pwani Khalid Shapi alisema kuwa hali hiyo inaathiri sio tu sekta ya utalii bali hata watumizi wengine wa kivuko hicho.

Hata hivyo, washikadau hao hawakuweka wazi kwa wanahabari maafikiano yao waliokubaliana kwenye kikao hicho baina yao na bodi hiyo.

Itakumbukwa kivuko cha feri kimekumbwa na utata wa kuharibika kwa feri zilizofanya msongamano wa abiria na magari mwezi uliopita.