Share news tips with us here at Hivisasa

Waziri wa Utalii Najib Balala amesema serikali imetenga shilingi bilioni 5.2 zitakazotumika kuimarisha sekta ya utalii na kuinua viwango vya kibiashara nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kibiashara na wadau wa sekta ya utalii mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Bw Balala alisema juhudi za serikali kuimarisha sekta hiyo ni kuhakikisha kuwa maswala ya kibiashara, uchumi na uwekezaji unatekelezwa ili kuona changamoto za kiuchumi zinatatuliwa.

Akiwasuta viongozi wa kisiasa, Balala alisema wakati umefika sasa kwa viongozi wa kisiasa kukoma kurushiana cheche za maneno hadharani ambazo huenda zikaathiri uchumi wa nchini na badala yake kuungana na kuwatekelezea wakenya maendeleo.

“Napenda kuwaambia viongozi wa kisiasa kuwa huu sio wakati wa siasa na waungane na kuwatekelezea wakenya maendeleo ili changamoto ambazo wakenya wanapitia kutatuliwa kwa ushirikiano," alisema Balala.

Aidha aliwataka kuwa katika mstari wa mbele kutafuta suluhu la kusitisha changamoto ambazo serikali inapitia badala ya kukosoa kila wakati ikizingatiwa kuwa kuimarika kwa uchumi wa nchi ni lazima kwa viongozi kushirikiana.

Waziri huyo wa utalii nchini alishikilia kuzidisha juhuzi za kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ili kuona kwamba sekta hiyo inafaulu katika kuwavutia wageni kuzuru humu nchini.