Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mke wa mshukiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la waislamu CIPK, sheikh Mohamed Idris amekanusha madai kuwa kulipatikana bunduki na vilipuzi chini ya godoro la kitanda chao.

Akitoa ushahidi huo siku ya Ijumaa katika mahakama kuu ya Mombasa, Asha Khalifa alisisitizia mahakama kuwa madai yanayomkabili mmewe si ya kweli, bali ni njama ya kumuangamiza mumewe kutohudumia familia yake.

Aisha alitokwa na machozi alipokuwa akielezea mahakama jinsi alivyopigwa kofi na polisi pasi sababu yoyote wakati alipotaka kujua kisa kinachomkumba mmewe Mohamed Soud.

Aidha, ameitaka mahakama kumwachilia huru mmewe ili apate kuhudumia mahitaji ya familia yake inayokumbwa na matatizo toka kutiwa mbaroni tangu mwaka 2014.

Mwezi Disemba mwaka 2015, Mshukiwa huyo aliwalaumu maafisa wa usalama kwa kumhusisha na mauwaji hayo, umiliki wa bunduki na kilipuzi, ikizingatiwa hana ujuzi wa kutumia silaha hizo hata kidogo.

Aidha, aliongeza kuwa maafisa wa usalama walimfunga kitambaa kha macho na kumzungusha kwa vituo kadha vya polisi kwa takrbani masaa manane, na kumwacha bila chakula, jambo alilolitaja kama kinyume cha haki za binadamu.

Mnamo Juni 10,2014, Mohamed Soud anadaiwa kuhusika katika mauwaji ya marehemu Sheikh Mohamed Idris katika eneo la Likoni.