Mwenyekiti wa ODM katika eneo bunge la Nakuru Magaribi Shem Osiago amesema mpango wa kutaka kiongozi kutoka chama kimoja aweze kuchangia na kuendeleza sera za chama kingine ni kuhujumu demokrasia.
Akizungumza siku ya Jumatatu, Osiago alisema mpango huo unaopendekezwa na mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu sheria Samuel Chepkonga, unarudisha nyuma maendeleo.
Aidha aliwataka wabunge wasiupitishe mswaada huo bungeni.
Kadhalika Shem alisema iwapo mswaada huo utapitishwa bungeni, itakuwa vigumu kwa upinzani kuikagua serikali.
Kutokana na hilo alieleza hofu yake kwani huenda ikaongeza visa vya ufisadi nchini.
Aidha upande wa msajili wa vyama vya kisiasa hapa nchini Lucy Ndung’u ni kuwa ni wajibu wa chama cha kisiasa kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi anayekiuka sheria za chama , wala si wajibu wa msajili wa vyama kuchukua hatua dhidi ya wale wanaokiuka mwongozo wa vyama.