Shirika la kutetea haki za binadamu la Centre for Enhancing Democracy and Good Governance CEDGG limetoa wito kwa majaji fisadi kuondoka afisini.
Katika kikao na wanahabari, mratibu wa mipango katika shirika hilo Masese Kemunche alisema kuwa majaji fisadi hawafai kuendelea kuhudumu.
"Ni jambo la kusikitisha kwamba hata idara ya mahakama imeingiwa na shtuma za ufisadi na langu ni kuomba tu majaji na mahakimu fisadi kujiondoa" Masese alisema.
Alikuwa akigusia swala la jaji Philip Tonui kushtumiwa kwa maswala ya ufisadi.
Wakati huo huo, amesema kuwa wakati ni sasa kwa idara ya mahakama kujisafisha.
Alisema kuwa,haitakuwa rahisi kwa wakenya kurejesha imani yao kwa idara hiyo.