Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika la usafir nchini  limeombwa kuingilia kati nyongeza ya nauli ambayo abiria huongezewa kila wakati na wahudumu wa matatu.

Wito huo umetolwa baada ya wahudumu hao wa matatu mjini Kisii kuongeza nauli kupita kiasi kuelekea sehemu mbalimbali huku shule zinapoendelea kufunguliwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii, abiria wengi, wakiongozwa na Samuel Orina waliomba shirika la NTSA kutoa msaada kwao dhidi ya kuongezewa nauli wanapoendelea kuwasafirisha watoto wao shuleni.

“Kila msimu shule zinapofunguliwa tunapata kibarua kigumu sana kwa kuongezewa nauli. Tunaomba NTSA kuingilia kati ili kutusaidia na nauli iweze kuwa kama kawaida,” alisema Orina.

Miongoni mwa sehemu ambazo abiria wanalalamikia dhidi ya kuongezewa nauli hiyo ni Kisii-Nairobi, Kisii-Mombasa, Kisii-Kericho, Kisii-Nakuru na Kisii Eldoret.

Wakati huo huo, abiria hao wamewataka wahudumu wa magari kuzingatia sheria za barabarani wanapofanya usafiri wao kwani imebainika kuwa wengi huendesha magari kiholela na hata kusababisha ajali barabarani.

“Tunaomba wadereva kuwa waangalifu na kuzingatia sheria za barabarabani wanapofanya uchukuzi wao maana huu ndio wakati tunasafirisha watoto kuelekea shuleni,” alisema Jenifer Makori, abiria.

Jukumu ni la shirika la NTSA kufuatilia malalamishi ya abiria na maafisa wa traffiki kuhakikisha madereva huzingatia sheria za barabarani.