Kamati ya uchukuzi katika bunge la kitaifa imesema itakutana na wakuu wa shirika la SECCO, jijini Mombasa kujadili iwapo wataweza kuboresha huduma za feri kupitia shirika hilo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Maina Kamanda aliyasema haya siku ya Ijumaa baada ya kukutana na bodi ya shirika la feri kujadili matatizo ya mara kwa mara ya kivuko hicho.
Maina alisema kuwa shirika la Secco lilionyesha mfano mzuri, na ana imani nalo baada ya shirika hilo kutengeneza feri mpya tena ya kwanza nchini iliyosafirishwa hadi ziwa Victoria.
Maina aliongeza kuwa ni sharti suluhu la haraka na la kudumu kutafutwa katika uboreshaji wa shirika hilo.
Aidha, meshinikiza kauli ya katibu wa kudumu katika uchukuzi John Mosonik kwamba wakuu wa kivukio hicho watachunguzwa na tume ya maadili na kupambana na ufisadi.
Haya yanajiri kutokana kushudiwa matatizo ya mara kwa mara katika kivuko hicho ambacho ndio cha pekee kinacho tumiwa na maelfu ya abiria kila siku.