Biwi la simanzi lilitanda mapema Ijumaa katika ufuo wa maiti wa War Memmorial mjini Nakuru wakati wa kuondolewa kwa mwili wa Justus Kiplang'at Ng'eno, aliyeaga dunia tarehe 24 Januari kutokana na tatizo la moyo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi wa shule hiyo ya Moi mjini Nakuru waliongozwa na mwalimu mkuu Stephen Karanja kutoa heshima zao za mwisho kwa mwendazake ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu. 

Na akizungumza katika eneo la Ngata wakati wa hafla ya mazishi ya mwendazake, mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Moi Stephen Karanja alimtaja mwendazake kuwa mwanafunzi aliyejitolea na mwenye bidii darasani.

Alisema kuwa jamii ya shule hio itazidi kuikumbuka familia ya mwendazake katika hali zote. 

"Justus alikuwa mwanafunzi mpole na mwenye bidii, na kwa niaba ya shule ya sekondari ya Moi ningependa kutoa rambirambi zetu na kwa familia tuzidi kuwakumbuka katika maombi" alisema Mwalimu Karanja. 

Hafla hio ya mazishi iliongozwa na kanisa la kianglikana huku mahubiri yakitolewa na kasisi Kambo ambaye alihimiza umuhimu wa maombi.