Shule ya sekondari ya King David katika eneo bunge la Bahati itageuzwa kuwa ya mabweni kwani mazingira yake yanatosha kwa hatua hio.
Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amesema kuwa shule hiyo itapigwa jeki katika miundo msingi ili kuinua viwango vya elimu.
"Tutahakikisha tunaimarisha madarasa na hata mabweni ili tuinue viwango vya elimu eneo hili," alisema Ngunjiri.
Alikuwa akizungumza wakati wa kupeana hundi ya shilingi laki saba kwa ajili ya ujenzi wa darasa shuleni humo siku ya Alhamisi.
Aidha alisema kuwa kugeuzwa shule hiyo kuwa ya mabweni kutasaidia pakubwa wanafunzi kutoka eneo la Bahati na Ol-Kalou katika kaunti ya Nyandarua.
Wakati huo huo, Ngunjiri amesema kuwa atafadhili ujenzi wa vyoo hasa ikizingatiwa kwa sasa wanafunzi wanatumia vyoo pamoja na wale wa shule ya msingi ya Kanduruma.