Shule zote za msingi na za upili katika kaunti ya Kisii zimeombwa kuajiri wafanyikazi wa kusimamia maktaba za shule hizo ili kutoa huduma bora za masomo kwa wanafunzi.
Hii ni baada ya kubainika kwa wasimamizi wengi wa maktaba za shule mbalimbali huwa walimu ambao hawawezi kutoa huduma bora kwani wakati mwingine huenda kufundisha wanafunzi darasani.
Akizungumza siku ya Jumanne katika shule ya msingi ya Nyakorere wakati wa hafla ya kuwa vitabu, mwakilishi wadi ya Boikang’a Elkanah Nyandoro alisema ili kutoa huduma bora kwa wanafunzi wanapoenda kwa maktaba ata wakati wa wikendi, sharti mfanyikazi aajiriwe ili kusimamia maktaba na kufuingua kila siku.
“Naomba kila shule iwe na msimamizi wa maktaba, kando na kuwa mwalimu, maana wakati mwingine huhamishwa hadi shule ingine na wakati mwingine maktaba haifunguliwi baada ya kuwa na shughuli nyingi za kufanya kwa kufundisha wengine darasani," alisema mwakilishi huyo.
Wakati huo huo, Nyandoro aliomba kamati hizo za shule katika kaunti ya Kisii kushirikiana pamoja kuhakikisha viwango vya elimu vinainuka.