Raymond Komen, aliyekuwa mkuu wa wafanyikazi kwenye kaunti ya Nakuru, ameteta kuwa gavana Kinuthia Mbugua alichochewa kisiasa ili kumfuta kazi.
Komen alisema to fauti zake na MCA wa Solai zilifanya afutwe kazi.
“Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa MCA wa Solai bwana Chebor nifutwe kazi,” Komen alisema.
Aidha Komen alisema kumekuwa na baadhi ya maafisa wa serikali ya kaunti hiyo ambao hawajafurahishwa na juhudi zake za kupinga miradi Fulani aliyoshuku inakumbwa na ufisadi.
“Hatua yangu kupinga kuhamishwa kwa ujenzi wa eneo la hospitali kutoka Salgaa hadi kwenye hospitali kuu ya kaunti pia kuliwafanya watu kunichochea nifutwe kazi,” Komen alisema kwenye taarifa.
Hata hivyo, serikali ya kaunti hiyo imesisitiza kuwa Komen alifutwa baada ya kususia kazi kwa miezi kadhaa.