Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amelaumu upinzani kwa kukosoa serikali kwa misingi isiyokuwa na maana.

Mbuvi alisema siku ya Jumamosi katika eneo la Shika Adabu kuwa serikali ya Jubilee imejitahidi pakubwa katika kuleta maendeleo ya taifa, kinyume na serikali zilizopita.

Aidha, ameulaumu mrengo wa Cord kwa kujaribu kupinga juhudi za serilkali katika kutatua mizozo ya ardhi nchini, na kusisitiza kuwa jambo hili halifai kuingizwa siasa.

Vile vile ameongeza kuwa upinzani ulihusika pakubwa katika unyakuzi wa ardhi na ufisadi, na badala yake Cord inaisingizia serikali ya Jubilee lawama hilo.

Sonko ameutaka upinzani kushirikiana na serikali katika kuendeleza uchumi wa taifa kwa manufaa ya mwananchi.

Wakati huo huo Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye ni mwanachama wa Cord amejitenga na madai hayo na kusema kuwa uongozi wake hauwezi jihusisha na wizi wa mali ya umma.