Wanachama wa ODM eneo bunge la Likoni wamemtaka Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi kumwomba msamaha Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, baada ya kumkemea na kumuhujumu mbele ya wakazi wa Mombasa katika eneo la Shika Adabu siku ya Jumamosi
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa chama hicho, mwenyekiti wa ODM eneo bunge la Likoni Hamisi Ali alionyesha kusikitishwa kwake jinsi senetaa alivyomkosea heshima Gavana Joho.
Aidha, amemtaka Sonko kuomba msamaha chini ya masaha 24 kwa Joho na wananchi wa Kaunti ya Mombasa kwa ujumla.
Domoko amekitaja kitendo hicho kama ya ukosefu wa nidhamu, na kumtaka Sonko kuheshimu viongozi wa kaunti zingine.
Siku ya Jumamosi katika mkutano uliohudhuriwa na Rais Kenyatta katika eneo la Shika Adabu, Sonko alimshambulia kwa maneno makali yanayodaiwa kuzua chuki na kumdhalilisha Gavana wa Mombasa.