Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Chache Richard Tong’i amepongezwa kwa kununulia shule ya upili ya st Paul Augustine Otamba Basi la shule kupitia pesa za hazina ya ustawi maeneo bunge CDF.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Alhamisi katika shule hiyo ya Otamba iliyoko eneo bunge la Nyaribari Chache baada ya mbunge huyo kukabidhi shule hiyo Basi hilo mpya, wengi wa wazazi hao walimpongeza mbunge wao kwa hatua hiyo. 

Kulingana nao, Tong’i aliwapunguzia mzigo wa kulipa pesa kila mara ili kutumika kukomboa basi wakati wanafunzi wanapokuwa na ziara ya michezo na masomo.

“Tunampongeza mbunge wetu kwa yale anaendelea kufanya katika eneo bunge letu hapa Nyaribari Chache,” alisema Christopher Ombwori mzazi wa shule hiyo.

“Tumekuwa tumesumbuka sana kwa muda mrefu kwa kuitishwa pesa kila mara ili kutumika kukomboa basi la kuwasafirisha wanafunzi wanapokuwa na ziara ya masomo na michezo lakini sasa tumepata afueni kupitia mbunge wetu,” alisema Jenifer Monari, mzazi mwingine.

Tong'i alikabidhi shule hiyo basi jipya siku ya Alhamisi na kusema ameratibu shule tatu ambazo zitafaidika na basi hivi karibuni ila tu hakusisema majina.

Shule ya Otamba ndio imekuwa shule ya pili katika eneo bunge hilo la Nyaribari chache kupokezwa basi baada ya shule ya upili ya Bobaracho.