Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeombwa kuongeza vituo vya kusajili wapiga kura hadi vituo vitano kwa kila wadi ili kusajiri idadi kubwa ya wapiga kura nchini.
Wito huo umetolewa baada ya tume hiyo kutangaza kuwa kila wadi itakuwa na kituo kimoja cha kusajili wapiga kura jambo ambalo limepingwa kwani wengi wa wananchi hawatapata fursa ya kujisajili.
Akizungumza siku ya Jumapili katika eneo bunge la Bobasi, mwenyekiti wa chama cha TNA katika eneo bunge hilo Yobesh Onchiri aliomba tume hiyo kuongeza vituo hivyo ili kusajiri idadi kubwa.
Kulingana naye, kuna baadhi ya wadi ambazo ni kubwa zaidi na kituo kimoja cha kusajili wapiga kura hakitaweza kwani wengine hawatatembea mbali kutafuta kituo hicho ili kusajililiwa kama wapiga kura
“Naomba tume ya IEBC kuongeza vituo hadi vitano kwa kila wadi ili kupeana fursa kwa watu wengi kusajiriwa kama wapiga kura,” alisema Onchiri
“Kuna wadi ambazo ziko kubwa na watu hawatatembea mbali ili kutafuta kituo cha kusajiri wapiga kura, sharti tume hiyo ione jinsi itafanya ili kusajiri watu wengi ambao watapiga kura,” aliongeza Onchiri.
Aidha, mwenyekiti huyo aliomba watu kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa ili kupata fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi wale watakaoleta maendeleo nchini.