Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Ubalozi wa India humu nchini unaitaka serikali kuwaachilia kwa dhamana wanafunzi wawili wa India walionaswa kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya katika meli ya Mv Amin Darya iliyozamishwa baharini mwaka jana.

Ubalozi huo, kupitia wakili wake Gichena Bw’ Omwando, uliwasilisha ombi hilo siku ya Jumatano la kutaka kupewa dhama kwa wanafunzi hao ili wakamalize masomo yao nchini India.

Gichena aliambia mahakama kuwa ubalozi huo umepata wadhamini wawili ambao watasimamia dhamana ya wateja wake humu nchini kwa mujibu wa katiba.

Ombi hilo litasikilizwa Disemba 2 mwaka huu baada ya kukosekana mkalimani wa Lugha ya Kihindi siku ya Jumanne.

Wawili hao ni Prabhakere Prwveen na A. Vikea pamoja na raia tisas wa kigeni kutoka Pakistan na watatu kutoka Kenya, ambapo wanadaiwa kunaswa na dawa za kulevya bandarini Mombasa zenye thamani ya shilingi bilioni 1.3.

Alhamisi iliyopita, mkuu wa polisi wa kituo cha Kilindini, Simon Simotwa aliambia mahakama kuwa uchunguzi wa kwanza uliofanywa kwa meli ya MV Amin Darya iliyolipuliwa baharini mwaka jana ulionyesha meli hiyo haikuwa na dawa za kulevya kama ilivyodaiwa.