Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Uchaguzi mdogo wa Malindi umetajwa kuvuruga sekta ya utalii maradufu katika eneo hilo.

Kauli hii ilitolewa siku ya Jumamosi na Gavana wa kaunti ya Mombasa, Hassan Joho, kwa kusema kuwa idadi ya watalii katika eneo hilo imepunguwa pakubwa kutokana na siasa za zinazoendelea katika sehemu hiyo ya Malindi.

Haya yanajiri wakati kunashuhudiwa joto la kisiasa katika eneo hilo, ambapo uchaguzi mdogo unatarajiwa mwezi Machi.

Aidha, aliongeza kwamba kuna haja ya Wakenya kuungana kwa minajili ya kuleta demokrasia sawia na kukomesha dhuluma za kihistoria na kuboresha utalii .