Share news tips with us here at Hivisasa

Uchaguzi wa kuwachagua viongozi katika nyadhifa mbalimbali wa chama cha ODM eneo bunge la Bomachoge Chache kaunti ya Kisii ulihairishwa kufuatia sababu ambazo hazingeweza kuepukika.

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike katika kaunti nzima ya Kisii siku ya Jumapili ili kuwachagua viongozi ambao watakiendesha chama hicho katika maeneo bunge nane ya kaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumapili katika eneo bunge la Bomachoge Chache, mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kisii John Nyang’au alitangaza uchaguzi huo kuhairishwa hadi Desemba tarehe 14 na 15 kwa kile alichokitaja kama sababu ambazo hazingeweka kuepukikika.

Tarehe hizo za kuandaaa uchaguzi huo tena ziliafikiwa baada ya gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae, Naibu wake Joash Maangi, mbunge wa eneo bunge hilo Simon Ogari na bodi ya kusimamia uchaguzi huo kuwa na kikao hichob siku ya jumapili na kupitisha tarehe hizo kuwa tarehe za kuandaa uchaguzi huo baada ya kuhairishwa .

“Katika maeneo mengine nane katika kaunti ya Kisii kura za kuwachagua viongozi umekamilika vizuri bila shida yoyote, lakini hapa Bomachoge Chache kura hizo zimehairishwa hadi tarehe 14 na 15 mtawalia mwezi wa Desemba kufuatia sababu ambazo hatuwezi kuzitaja. Naomba wananchi kuwa watulivu hadi wakati huo,” alisema Nyangau.

Aidha, mwenyekiti wa chama hicho cha ODM mkoani Nyanza Peter Odoyo alisema nafasi mbili zitatengewa wale watachaguliwa katika eneo bunge hilo baada ya kuchaguliwa kwa kukiendesha chama cha ODM.